Wakati Sheikh
Abu Al-Hassan Ali Khabbaz عَـلَيْهِ
رَحْـمَةُ الْـمَنَّانْ alipo simuliwa ule mkasa wa wale ngamia
waliopotea, alisema kwamba yeye aliwahi kuambiwa na Sheikh Abu al-Qasim
عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الْـمَنَّانْ kwamba alimsikia Sheikh ‘Abdul-Qadir Jilani
عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ
الۡـقَـوِی akisema,
‘Yule atakae omba msaada wangu katika shida na dhiki basi atapata uokovu wa
shida hiyo na atakae nitaja mimi katika muda wa taabu basi atapata nafuu ya
taabu hiyo. Yeyote amuombaye Allah عَزَّوَجَلَّ chochote kwa kulitaja jina langu, basi haja yake
itatimizwa.’
Mtu atakae sali rakaa mbili za nafli, katika kila rak'at akasoma suratul Ikhlas mara 11 baada ya suratul fatiha na baada ya kutoa salamu amsalie Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم kisha aelekee hatua 11 kwenda Mji Mtukufu wa Baghdad na kuomba shida zake na aombe kutatuliwa haja yake عَزَّوَجَلَّ haja yake itatimizwa.’
(Bahjat-ul-Asrar, uk. 197)
صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد
Ndugu zangu waislamu! Baada ya kusoma matukio yaliyopita, mtu anaweza kufikiri kwamba ni lazima kuomba msaada kwa Allah عَزَّوَجَلَّ yeye pekee na hakuna mwengine zaidi yake kwa sababu wakati Allah عَزَّوَجَلَّ ana mamlaka ya kutoa msaada, kwa