Mfalme wa majini

Nabii Issa alipowaambia wafuasi wake, ‘Ni nani wasaidizi wangu kwa (ajili ya kutangaza dini ya) Allah?’ wafuasi wakasema sisi ni wasaidizi wa (kutangaza dini ya) Allah.

(juzuu 28, Sura Saf, aya 14)

Sayyidunā Musa عَـلَيْـهِ الـسَّـلاَم ameomba msaada kutoka kwa watu

Wakati Sayyidunā Musa عَـلٰى نَبِـيِّـنَا وَ عَـلَيْـهِ الـصَّلٰوة ُ وَالـسَّلَام alipotakiwa kwenda kumlingania Firauni, alimuomba Allah عَزَّوَجَلَّ ampatie msaada wa mwanadamu na kumuomba Allah عَزَّوَجَلَّ kama ifuatavyo;

وَ  اجۡعَلۡ   لِّیۡ    وَ زِ یۡرًا  مِّنۡ   اَہۡلِیۡ  ﴿ۙ۲۹﴾    ہٰرُوۡنَ   اَخِی   ﴿ۙ۳۰﴾    اشۡدُ دۡ   بِہٖۤ   اَزۡرِیۡ   ﴿ۙ۳۱﴾

‘Na unifanyie waziri katika jamaa zangu, ndugu yangu Haruni (mfanye awe ndie waziri wangu) nitie nguvu kwa (ndugu yangu) huyu’ (Juzuu ya 16, Sura Taha, Aya 29-31)

Wacha Mungu pia wanasaidia

Allah عَزَّوَجَلَّ amesema mahali pengine:

فَاِنَّ  اللّٰہَ   ہُوَ   مَوۡلٰىہُ   وَ  جِبۡرِ یۡلُ

وَ صَالِحُ   الۡمُؤۡ  مِنِیۡنَ ۚ   وَ الۡمَلٰٓئِکَۃُ    بَعۡدَ   ذٰلِکَ  ظَہِیۡرٌ      ﴿۴﴾

 

Index