Mfalme wa majini

Ielekeze kata usawa wa Qiblah

Enyi wafuasi wa Sultani wa Baghdadi! Bila shaka, mapenzi ya dhati kabisa ni kufuata kila kitendo cha yule umpendae. Hivyo basi kama inawezekana kuielekeza kata ya kutawadhia upande wa Qiblah basi  fanyeni hivyo hivyo. Muhadithi-al- A'zam Maulana wa Pakistani Sheikh Sardar Ahmad رَحْمَةُ اللهِ تَعَالٰی عَلَيْه alikuwa anaielekeza kata yake ya kutawadhia na viatu vyake upande wa Qiblah na mimi Sag-e-Madīnaĥ (mwandishi) huwa nafanya bidii kuzifuata nyayo walizopita wacha Mungu kama hawa (رَحِمَهُمُ الـلّٰـهُ تَـعَالٰی) kwa kuielekeza kata yangu na viatu vyangu upande wa Qibla, bali napenda kila kitu kielekee Qibla.

Kisa cha Yule aliyekuwa na tabia ya kuelekea Qiblah

Ndugu waislamu! Kadri inavyowezekana, tunatakiwa kuendeleza tabia ya kukielekea Qiblah kwa sababu kuna baraka nyingi za kufanya hivyo. Sheikh Imam Burhan-ud-Dīn Ibrahim Zarnūjī رَحْمَةُ اللهِ تَعَالٰی عَلَيْه anasimulia; ‘Wanafunzi wawili walisafiri nje ya nchi kutafuta utambuzi wa maarifa ya dini. Wote wawili walikuwa katika darasa moja. Wakati waliporudi nyumbani, mmoja wao alikuwa mwanachuoni mkubwa sana na mwengine akabakia kuwa ni mjinga. Wanazuoni wa mji ule wakaanza kufikiria sababu gani iliyowafanya kuwa tofauti. Baada ya kufanyika uchunguzi wa makini katika njia zao za kujifunza, namna zao

Index