Sheikh Bishr Qarzī عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡـقَـوِی amesema, ‘Siku moja nilikuwa (nasafiri) na msafara wa biashara wa ngamia 14 waliobeba sukari. Sote tukakaa katika kambi ndani ya msitu wenye kutisha katika usiku ule. Katika sehemu ya kwanza ya usiku ule, ngamia wetu wane tuliowabebesha sukari wakawa wamepotea. Licha ya juhudi zangu za kuchoka sikuwaona. Msafara ukaondoka na ukaniwacha mimi pamoja na muendesha ngamia wangu.
Asubuhi iliyofuata, mimi nilikumbuka kwamba Murshid wangu, Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم mara moja aliwahi kuniambia, ‘Muda wowote ambao itakukumba shida au tabu liite jina langu, wewe utakuwa ni mwenye kuondokewa na shida uliyonayo.’ Kwa hiyo, mimi nikaanza kuomba msaada nikisema, ‘Ewe Shaykh 'Abd-ul-Qadir! Mimi nimepotelewa na ngamia wangu!’ Hapo hapo akanijia mcha Mungu, akiwa na nguo nyeupe, amesimama juu ya kilima kidogo upande wa mashariki. Yule mcha Mungu akatoa ishara na mimi na muendesha ngamia wangu tukaanza kumfuata na kumsogolea, tulianza kumkaribia akatupotea machoni mwetu. Tukaanza kuangalia kila mahala kwa hali ya mshangao na kuchanganyikiwa kabisa. Ghafla, tukawaona wale ngamia wetu wane wamekaa chini ya bonde. Tukaenda kuwakamata na tukaongoza kwenda kuufuata ule msafara.’
(Bahjat-ul-Asrar, uk. 196)