Sheikh Umar
Bazar عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الْـمَنَّانْ amesema,
‘Ijumaa moja, nilikuwa naelekea katika msikiti pamoja na Ghaus-e-A’zam
عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم. Mimi niliwaza moyoni kwamba ni jambo la
ajabu kabisa kwamba kawaida ninapoenda msikitini siku ya Ijumaa pamoja
na Murshid wangu, watu wengi wanakusanyana karibu yetu na kuanza kumtolea
salamu na kumpa yeye mikono hadi inakuwa vigumu sana kuendelea na matembezi
yetu; lakini leo hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa na khabari juu yake. Basi
baada ya lile wazo kunipitikia ndani ya moyo wangu palepale Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم akaniangalia kwa tabasamu.
Ghafla, watu wakaanza kumkimbilia na kupeana mikono na Sultani wa baghdadi عَـلَيْهِ رَحۡمَةُ الـلّٰـهِ الۡـهَادِی. Kukawa na watu wengi waliosongamana na walituzonga mimi na yeye Murshid wangu عَـلَيْهِ رَحۡمَةُ الـلّٰـهِ الۡـهَادِی mpaka mimi nikasema tena moyoni kwamba ilikuwa bora mwanzo. Mara tu wazo hili liliponipitikia moyoni mwangu, yeye رَحْمَةُ اللهِ تَعَالٰی عَلَيْه alisema, ‘Ewe Umar! Ilikuwa ni wewe ndie ulie utamani umati wa watu. kwani si unajua kwamba nyoyo za watu zipo katika kiganja changu! Nikitaka nitawafanya wanifuate na nikitaka naweza kuwafanya wasinifuate.’ (Bahjat-ul-Asrar, uk. 149)
Kunjiyān dil kī Khuda bali Tujhay din Aisi kar,
Ke Yeh Sina ho mahabbat ka khazanah tayrā
Allah amekupa funguo za nyoyo katika mkono wako
Ufanye moyo wangu uwe hazina ya mapenzi yako