‘Basi kwa hakika Allah ndiye msaidizi wake na Jibril na waislamu wema, na zaidi ya hayo pia Malaika watasaidia.
(Juzuu ya 28, Sura Tahrim, aya 4)
Ndugu muislamu, umeshaona? Kwamba Quran imeshatangaza wazi kuwa Allah عَزَّوَجَلَّ ni kweli Msaidizi lakini kwa fadhila zake Allah عَزَّوَجَلَّ, Jibril na watu walio karibu na Allah عَزَّوَجَلَّ (Manabii عَـلَيْـهِمُ الـصَّلٰوة ُ وَالـسَّلَام na watu wema) na hata Malaika wanaweza kusaidia. اِنْ شَــآءَالـلّٰـه عَزَّوَجَلَّ Sasa ule wasiwasi wa shetani kwamba hakuna yeyote asiyekuwa Allah عَزَّوَجَلَّ anaeweza kutoa msaada ushaondoka kabisa. La kutia nguvu zaidi ni kwamba watu waliohamia madina wanaitwa Muhajir (masahaba waliohama) na wale walio wasiaidia na kuwaunga mkono ni Ansaar (masahaba waliosaidia) kila mtu aliesoma anaifahamu maana ya neno Ansaar kama ni wasaidizi.
صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد
Inawezekana kwa Shetani kumfanya mtu afikiri kwamba inaruhusiwa kuomba msaada kutoka kwa mtu hai lakini haijaruhusiwa kwa maiti. Kama utazisoma kwa makini aya zifuatazo na mada inayofuata hapo mbele basi huenda wazo baya la shetani likakutoka kabisa اِنْ شَــآءَالـلّٰـه عَزَّوَجَلَّ Inaelezwa kuwa: