Abu Saad ‘Abdallah Bin Ahmad alisema, ‘Mara moja, binti yangu Fatimah alitoweka kutoka katika paa la nyumba. Basi nikapatwa na wasiwasi na kwenda kupeleka mashtaka yangu kwa Sultani-ul-Auliya, Sheikh Ghauše-A'zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم na nikamtaka msaada. Akasema, عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡـقَـوِی ‘Nenda Karkh (mji) na kakae nyikani wakati wa usiku na tengeneza upweke uzio wa kiroho (yaani mduara) wewe na nafsi yako tu. Isome بِسۡـمِ الـلّٰـه na tafakari juu yangu. Katika nyakati za usiku, misafara mingi ya majini itapita karibu na wewe. Nyuso zitakushtua kwa ugeni uliokuwa wa ajabu sana lakini usitishike. Wakati wa alfajiri, mfalme wa majini atakuja kwako na atakuuliza nini shida yako. Basi utamwambia, ‘Sheikh ‘Abd-ul-Qadir Jilani عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡـقَـوِی amenituma mimi kutoka Baghdadi na nakutaka unitafutie binti yangu aliyepotea.’
Kwa maana hiyo, mimi nikatoka Karkh na
nikayafuata maelekezo ya Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم Ndani ya kile kiza cha usiku ule, majini
wenye kutisha wakawa wanapita kwenye uzio wangu. Nyuso zao zilikuwa ni za
kutisha kiasi kwamba sikuweza kuvumilia kuziangalia. Wakati wa alfajiri, mfalme
wa majini alikuja ilhali amepanda farasi pamoja na majini wengine. Alikuwa amebakia nje ya
uzio na kuniuliza mimi, ni ipi shida yangu. Mimi nikasema kwamba Ghaus-e-A’zam
عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ
الۡـقَـوِی alikuwa
amenituma kwake. Kusikia vile tu, akashuka farasi na kukaa chini. Majini wengine
wakafanya