hivyo hivyo wakakaa chini ardhini nje ya uzio wangu. Mimi nikampa taarifa kuhusu majanga ya yule binti yangu. Mfalme wa majini akatangaza miongoni mwa majini kwa kuuliza, ‘Ni nani aliyemteka nyara msichana?’ Muda mfupi tu, jini kutoka china alikamatwa na kuletwa mbele kama mhalifu. Mfalme akamuuliza, ‘Kwa nini ukamteka nyara msichana kutoka mji wa Qutb[1] wa zama hizi?’ Jini wa Kichina huku akitetemeka alijibu, ‘Mtukufu! Mimi nimempenda katika mara yangu ya mwanzo kumuona.’ Mfalme aliamuru kichwa cha yule jini wa Kichina kikatwe na binti yangu arejeshwe kwangu.
Kumshukuru Yule mfalme, nikasema, ‘Wewe ni mfuasi mkubwa wa Sheikh Ghaus-e-A’zam’ Akajibu: ‘Wallahi, عَزَّوَجَلَّ wakati Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم anapoanza kututazama tu, basi majini wote tunaanza kutetemeka. Na pindi tu Allah عَزَّوَجَلَّ akimteua Qutb, majini wote na wanadamu wanawajibika kumtii yeye.’ (Bahjat-ul-Asrar, uk. 140)
Mtu mmoja amesimulia tukio lililotokea katika Kutiyana (Gujarat, India), kijiji cha mababu wa Sag-e-Madīna (mwandishi). Kulikuwa na mtu katika Kutiyana (mji) ambaye alikuwa ana upendo mkubwa sana kwa Ghause-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم. Alikuwa akisherehekea Giyārĥwīn mara kwa mara. Tabia yake