msaada kutoka kwa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم katika kasida yake mashuhuri inayojulikana ‘Qasīdaĥ-e-Burdah’ na akasema: ‘Ewe mbora wa viumbe! Sina mwingine isipokuwa wewe, ambaye atanipatia msaada katika nyakati za shida.
(Qasīṣdaĥ-e-Burdah, uk. 36)
Imdādullāĥ Muhajir Makki عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الْـمَنَّانْ ameomba katika kitabu chake cha mashairi chenye jina 'Nālaĥ-e-Imdad:
Laga takyaĥ gunāĥaun Ka para din raat sautā Hun
Mujhay ab Khuwab-e-ghaflat se Jaga do Ya Rasulallah
Nina lala mchana na usiku juu ya mto wa madhambi
Niamshe mimi ewe Rasulallah kutoka katika ndoto za pumbao.
Siku moja, kundi la watu wacha Mungu رَحِمَهُمُ الـلّٰـهُ تَـعَالٰی kutoka kijiji cha Jīlān walitembelea mahakama yenye kheri ya Sheikh Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم na kuona kata (chombo cha kuchukua udhu) yake haikuwa imelekea Qiblah basi wakamfikishia taarifa Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم juu ya jambo hilo. Yeye رَحْمَةُ اللهِ تَعَالٰی عَلَيْه akamuangalia kwa jicho la ghadhabu mtumishi wake ambaye hakuweza kuvumilia hali ya ukali wa Sheikh kwa kuangaliwa kule na akaanguka chini na akatetemeka mpaka akafariki. Kisha Ghaus-e-A’zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم akaitazama kata yake, basi ile kata yenyewe ikaelekea Qiblah. (Bahjat-ul-Asrar, uk. 101)