Mfalme wa majini

nyengine ni kwamba alikuwa akionyesha utiiifu mkubwa na heshima kwa Masayyid. Alikuwa mkarimu sana na mwenye kuwajali sana hata watoto wa masayyid, kiasi kwamba akiwaona tu, anawanunulia pipi tamu.

Alipofariki duniani, kiwiliwili chake kilikuwa kimefunikwa na kitambaa na watu walikuwa wamekaa pembeni mwake kwa huzuni lakini ghafla, yule mfuasi wa kweli wa Ghaus-e-A’zam akainuka na kukaa kitako. Watu wakawa na khofu na waliachwa na mshangao, wakataka kukimbia.

Akawaita na kusema, ‘Musiogope, nisikilizeni mimi!’ watu walipokuwa karibu nae akasema, ‘Nawaambieni ukweli kwamba sasa hivi Murshid[1] wangu, Sheikh ‘Abd-ul-Qadir Jilani عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم amenitunukia uwepo wake na ameniambia, ‘Mfuasi wangu umefariki bila ya kutubia! Haya inuka upesi utubie.’ Roho yangu ikarejea katika kiwiliwili changu ili nije kufanya toba. Baada ya kusema hayo, akaomba msamaha wa madhambi yake na akaitamka kalima.

Hongereni wafuasi wa Ghaus-e-A’zam kwa sababu Sultani wa Baghdadi عَـلَيْهِ رَحۡمَةُ الـلّٰـهِ الۡـهَادِی amesema, ‘Mfuasi wangu, hata awe ametenda madhambi kiasi gani, basi hatafariki mpaka afanye toba.’ (Bahjat-ul-Asrar, uk. 191)

 



[1] mwongozo wa kiroho

Index