Mfalme wa majini

Ni sunna kwa Muballighīn na walimu kuwa wao wakipe mgongo Qibla ili wasikilizaji (wanafunzi) waweze kukaa ilhali wameelekea Qiblah. Ndio maana, Sheikh Hafidh Sakhāwī رَحْمَةُ اللهِ تَعَالٰی عَلَيْه amesema, ‘Sababu moja wapo kwamba kwanini Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم alikuwa akikipa mgongo Qiblah, ilikuwa ni kuwaruhusu masahaba waelekee Qiblah.

(Al-Maqasid-ul-hasanah, uk. 88)

Sayyidunā ‘Abdullah Bin Umar رَضِیَ الـلّٰـهُ تَعَالٰی عَـنْهُمَا mara kwa mara alikuwa anaelekea Qiblah. (Al Adab al Mufrad, uk 291 , Hadithi 1137)

Wakati wa kufundisha Qur'ani Tukufu na elimu, unapaswa kukaa ilhali umekipa mgongo Qiblah kwa niya ya kutekeleza sunnah ili kuwawezesha wanafunzi kuelekea Qiblah. Na wanafunzi wafundishwe sunna, falsafa na nia ya kukaa katika utaratibu huu. Jaribu kukaa ilhali umelekea Qiblah utakapokuwa husomeshi darasani.

Wanafunzi wanapaswa kuelekea Qibla ikiwa katika kuelekea Qibla wanaweza kumuelekea mwalimu pia (kama haiwezekani basi wamuelekee mwalimu tu) la kama si hivyo itakuwa vigumu kumuelewa mwalimu.

 

Index