Mfalme wa majini

Ni sunna kwa Khatib kutoa khutba ilhali amekipa mgongo Qibla ili wale wanaomsikiliza wamuelekee yeye khatib.

Wakati wa kusoma Qur'an Tukufu, vitabu vya dini, kuandika Fatwa, kutunga kitabu, kuomba dua, kufanya Zikri, kumsalia mtume na wakati wowote ukiwa umekaa chini au umesimama, kama hakunakizuizi chochote kinacho husiana na dini, jaribu kujizoesha tabia ya kuelekea Qiblah kila wakati ili upate thawabu nyingi. (Ikiwa wewe umo ndani ya nyuzi 45 ya Qiblah utakuwa unahisabika kama umeelekea Qiblah).

Kama inawezekana, weka meza, kiti nk kuelekea usawa wa Qibla ili wakati wowote ukiwa umekaa utakuwa umeelekea Qiblah.

Kama imekutokea tu ukawa umeelekea Qiblah bila ya kukusudia hivyo basi hutapata ujira wowote. Hivyo basi mtu anatakiwa awe ananuwia nia njema, kwa mfano           (1) kupata thawabu ya akhera (2) kutekeleza sunna            (3) Ninaelekea Ka'abah kwa heshima yake na utukufu wake. Wakati unajisomea au kufanya utafiti wa vitabu vya Kiislamu na masomo mengine unapaswa kuweka nia kama hizo ikiwa ni pamoja na kwamba kwa kuitekeleza sunnah ya kuelekea Qibla, nitapata baraka ya elimu ya Dini.

 

Index