ya kujiunga na Silsilah ya Qadiriyya razawiyya. Ghafla nikapatwa na usingizi, basi macho yangu yalipo jifumba, niliona kwamba sheikh Ghaus-e-A'zam عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡاَکْرَم amekaaa na uso wake ni wenye kumemeta na amekitanda kishali chake, nikasogea mbele na nikakishika kwa upande. Na nikahisi kuwa kuna watu wengine pia wamekishikilia lakini sikuweza kumuona yeyote kati yao. Nikayakariri yale maneno yanayosemeshwa wakati wa bay'ah. Hapo hapo baada tu ya ile bay'ah kumalizika, nikapeleka maombi ya kuwa mke wangu ana mimba na anahisi maumivu makali sana. Na daktari ameshauri afanyiwe upasuaji; basi nipatiwe nafuu na janga hili. Akanijibu, ‘Tumia tiba ya Baghdadi.’ Nikauliza kwa heshima, Ewe Murshid wangu! Muda umeenda na ninatakiwa kuifanya usiku huu huu.’ Akanijibu, ‘Umeruhusika kuifanya katika mchana, kabla ya siku kumalizika na اِنْ شَــآءَالـلّٰـه عَزَّوَجَلَّ utabrikiwa watoto mapacha bila ya upasuaji. Wape watoto wako majina ya Hassan na Mushtaq. Wote hao wawili watakuwa chini ya uangalizi wangu.’ Nikafanya kama nilivyo amrishwa na nilimpatia mke wangu tende kama inavyotakiwa.
اَلْـحَمْـدُ لـِلّٰـه عَزَّوَجَلَّ! Majibu nikayaona hapohapo na yale maumivu yakapotea kabisa, na mke wangu akajifungua bila ya shoda yoyote ile. Ninashuhudia kuwa nilijaaliwa watoto mapacha wawili kama vile Ghauše-A'zam alivyo ni bashiria, na nikawapa majina ya Hassan na Mushtaq kama ilivyo agizwa.’